Wednesday, August 8, 2012

SCRIPT SAMPLE



 EXT.–BARABARANI-JIONI
Catty na rafiki yake Rose wanatembea barabarani kwa hatua za taratibu huku wakizungumza.
ROSE
Usinambie best,mama kafrahije?Maana alikuwa hapendi kabisa kujichanganya na watu wa uswahilini.Afu sijamuona kanisani!

CATTY
Wee acha mama yangu afrahi…kasema amechoka,nimemwacha bado kalala.

ROSE
(Anamgeukia rafiki yake)

Sipati picha maisha ndani ya mjengo mpya nini?

CATTY
Nyumba ni nzuri utakuja uione,pale pale mwambani kituoni wala huwezi kupotea. namshukuru Mungu kwa kweli,sikutegemea!

ROSE
(Anamgeukia rafiki yake)

Isije ikawa boss kakuzimia?

CATTY
Wee hamna hiyo… kwanza bosi wetu siye mwanamke.Wee njoo umuone mama,siku mbili tu ameanza kunenepa.

Rose anacheka,na kumgonga bega rafiki yake.Huku wakicheka wote wawili kwa pamoja wanageuka kuitazama gari inayopita,kisha wanaendelea.



ROSE
Bado siku chache tu tutakuona na wewe unadrive.

CATTY
(Anainua mabega kuonyesha inaweza kutokea)

Mungu akipenda, si unajua maskini haishiwi ndoto!

LONG SHOT:Gari ile ikiishiria kwa mbali.

No comments:

Post a Comment